Yesu ni Nani? Ni swali ambalo Wayahudi walikuwa nalo. Katika sura ya 9 ya Injili ya Yohana tunaona jinsi yule aliyezaliwa kipofu alivyoweza kumtambua Yesu kama Mwana wa Mungu ila Mafarisayo walishindwa. Tukishindwa kumfahamu Yesu mara nyingi hutokona na hali yetu na ugumu wa mioyo yetu si kwamba ni ngumu kumfahamu. Pia tunaona jinsi Yesu alitumia Jina la Mungu MIMI NIKO katika sura ya 8. Kwa kweli Yesu ndiye Masihi mwana wa Mungu.
Mafundisho haya yanaendana na masomo yanayopatikana katika Kozi ya Maji ya Uzima inayoitwa Hatua ya Kwanza.
Kwa maelezo zaidi kuhusiana na masomo haya au kujiunga na kozi wasiliana nasi kupitia
Barua pepe: neno@majiyauzima.com
Simu: +255754 490 549 / +255694 298 395 /+255719 275 767