Sisi ni Nani?

Maji ya Uzima ni kozi zinazokuwezesha kuwa msomi wa Biblia popote ulipo. Lengo kuu ni ujikuze kiroho. Yanatolewa bila malipo ya pesa.
Mradi huu wa maji ya uzima unatoa kozi mbalimbali kwa njia ya vitabu. Kozi ya kwanza inaitwa “HATUA YA KWANZA” inayotokana na injili ya Yohana. Utakapokuwa unaendelea na kozi, utatambua Biblia inasema nini kuhusu kuwa mkristo, kuyashinda majaribu, uhakika wa wokovu, uchumba na ndoa za kikristo, utengano wa kanisa na serikali, uaminifu katika kushughulikia pesa, kuishi kwa amani, kutembea na Mungu na mengine mengi.
Kujiunga, tafadhali jaza fomu kwa umakini kisha uitume kwa anuani ya hapo chini au upeleke kwenye kituo kilichopo karibu na wewe. Ubarikiwe
Kwa mawasiliano zaidi:
Kwa posta: Maji ya Uzima
                     Harmony International Foundation
                      s.l.p  1548, Mbeya Tanzania

barua pepe: neno@majiyauzima.com

simu: +255694 298 395/+255719 275 767 

Play Video