Katika sura ya 9 ya Injili ya Yohana tunasoma habari za mtu aliyezaliwa kipofu. Tunajifunza umuhimu wa kukubali hali yetu ya kuwa tu vipofu. Tunahitaji uponyaji wa kiroho tuweze kuona.
Kupata uponyaji huo tunapaswa Kufahamu hali yetu kwamba tu vipofu, Kutii na kumtawaza Yesu kama Bwana, na Kuamini yaani kujenga juu ya msingi wake. Katika Injili ya Yohana tunakuta neno kuamini mara 113. Bila Imani hatuwezi kumpendeza Mungu. Imani yetu itaonekana pia katika maisha yetu si tamko tu au jambo la moyoni.
Pia ndugu Jeff anatuhimiza kuchunguza Maandiko Matakatifu ili tufahamu kwa ufasaha zaidi msimamo wetu, tusidanganyike.
Mafundisho haya yanaendana na masomo yanayopatikana katika Kozi ya Maji ya Uzima inayoitwa Hatua ya Kwanza.
Kwa maelezo zaidi kuhusiana na masomo haya au kujiunga na kozi wasiliana nasi kupitia
Barua pepe: neno@majiyauzima.com
Simu: +255754 490 549 / +255694 298 395 / +255719 275 767