Tukimwamini Yesu wajibu wetu ni nini? Katika somo hili Mch. Justin anaangalia maanake kumfuata Yesu. Ni lazima tuwe tayari kumkiri Yesu. Kama vile katika sura ya 21 ya Injili ya Yohana Yesu anamwuliza Petro kama anampenda ili Petro akiri wazi kwamba anampenda. Sisi nasi hatuwezi kuwa na aibu katika kumfuata Kristo.
Mafundisho haya yanaendana na masomo yanayopatikana katika Kozi ya Maji ya Uzima inayoitwa Hatua ya Kwanza. Kwa maelezo zaidi kuhusiana na masomo haya au kujiunga na kozi wasiliana nasi kupitia Barua pepe: neno@majiyauzima.com Simu: +255754 490 549 / +255694 298 395 /+255719 275 767