18 Hatua ya Kwanza Somo 18-19; Yesu, Mkombozi Aliyesulubiwa

5 Oktoba, 2024

Kitabu: Yohana

Bible Passage: Yohana 19-20

Katika sura za 19-20 Injili ya Yohana tunashuhudia namna Yesu alikuwa mfalme. Si mfalme aliyetawala kwa nguvu na ubavu bali alishinda kwa kuuliwa. Pale alipoonekana kushindwa Yesu alishinda hapo hapo. Pia tunajifunza kuwa katika ufufuo Yesu ametangulia. Maana yeye ni wa kwanza kufufuka na mwili usio wa uharibifu. Tunaona pia kwamba Yesu ni Kristo, Mwana wa Mungu na ndio lengo lake Yohana kuandika Injili yake.

Katika Injili ya Yohana tunajifunza kuhusu Sifa za Yesu. Katika video hii Ndugu Mathew anarudia sifa zote tulizoziona katika vipindi vilivyopita.

Mafundisho haya yanaendana na masomo yanayopatikana katika Kozi ya Maji ya Uzima inayoitwa Hatua ya Kwanza.

Kwa maelezo zaidi kuhusiana na masomo haya au kujiunga na kozi wasiliana nasi kupitia

Barua pepe: neno@majiyauzima.com

Simu: +255754 490 549 / +255694 298 395 /+255719 275 767