8a Utiifu; (Tunatakiwa Kumtii Nani?) Madaraja ya Kumfikia Mungu

25 Aprili, 2025

Mungu anapenda utiifu kuliko sadaka na madhabahu. Wakati mwingine tunahisi tutafanya kitu kikubwa kwa ajili yake Mungu. Tunatoa pesa nyingi, tunahubiri, tunaenda kanisani mambo ambayo ni mazuri na muhimu. Lakini Mungu hasa anataka mtu ambaye yuko tayari kumtii. Ikiwa unaishi katika dhambi yale mazuri unayoyafanya hayana maana mbele za Mungu. Mungu ameweka viongozi katika maisha yetu. Kuwa na moyo wa unyenyekevu na kutii ndivyo Mungu anavyotaka kwa ajii yetu. Mch. Korosso anafundisha juu ya hayo pamoja na kukaribisha wengine kutoa mifano katika maisha yao juu ya maisha ya kutii hata katika mazingira magumu.

Mafundisho haya yanaendana na masomo yanayopatikana katika Kozi ya Maji ya Uzima inayoitwa Madaraja ya Kumfikia Mungu. Kwa maelezo zaidi kuhusiana na masomo haya au kujiunga na kozi wasiliana nasi kupitia

Barua pepe: neno@majiyauzima.com

Simu: +255754 490 549 / +255694 298 395 / +255719 275 767