Ushawahi kumwona mtoto anafanya kitu shingo upande? Labda kuna kitu unajua unatakiwa ufanye ila unachelewa kufanya. Pengine umewahi kushuhudia mtu aliyeagizwa jambo fulani ila anatekeleza nusunusu. Je! katika hali hizi kuna utii? Wakati mwingine tunasikia kwamba tunaokolewa kwa imani tu. Kama ni imani tu utii una sehemu gani katika maisha yetu? Labda unataka kumtii Mungu lakini umeshindwa. Mchungaji Korosso anajibu haya pamoja na maswali mengine katika somo hili.
Mafundisho haya yanaendana na masomo yanayopatikana katika Kozi ya Maji ya Uzima inayoitwa Madaraja ya Kumfikia Mungu. Kwa maelezo zaidi kuhusiana na masomo haya au kujiunga na kozi wasiliana nasi kupitia
Barua pepe: neno@majiyauzima.com
Simu: +255754 490 549 / +255694 298 395 / +255719 275 767