9a Kukua Kikristo; (Bado ni Mtoto Katika Bwana au Umekua?) Madaraja ya Kumfikia Mungu

15 Mei, 2025

Kitabu: Warumi

Bible Passage: Rum 12:1-2

Hatuoni shida kama mtoto mdogo hawezi kutembea au kuandika. Ila kama ataendelea bila kukua na kujifunza mambo haya tutakuwa na wasiwasi juu ya mtoto huyo. Inakuwaje basi kwamba baadhi ya Wakristo ni kama hawakui? Wewe je! Katika maisha yako ya Kiroho unakua? Kuna vikwazo gani ambavyo vinaweza kumfanya mtu asikuwi? Katika somo hili Ndugu Jason anatusaidia kuelewa zaidi na pia tunajifunza hatua ambazo zinaweza kutusaidia kukua pia.

Mafundisho haya yanaendana na masomo yanayopatikana katika Kozi ya Maji ya Uzima inayoitwa Madaraja ya Kumfikia Mungu. Kwa maelezo zaidi kuhusiana na masomo haya au kujiunga na kozi wasiliana nasi kupitia

Barua pepe: neno@majiyauzima.com

Simu: +255754 490 549 / +255694 298 395 / +255719 275 767