Bila shaka Mungu anataka tushinde. Na sisi pia tunataka kushinda. Kwa nini basi bado tunashindwa? Wakristo wengi wanashindwa kuishi maisha matakatifu. Katika somo hili ndugu Jeff anapitia somo la Ushindi na jinsi ushindi unavyopatikana. Kuna wengine wanafundisha kwamba kama umeokoka basi hakuna kurudi nyuma wala kupotea. Lakini Biblia inatuambiaje? Katika Ufu 3:21 tunasoma: “Yeye ashindaye, nitamridhia kuketi pamoja nami katika kiti changu cha enzi, kama mimi nilivyoshinda nikaketi pamoja na Baba yangu katika kiti chake cha enzi.” Katika Biblia tunakuta kwamba kuna kuanza lakini kuna kumaliza pia. Tusipomaliza tutaweza kweli kuketi pamoja na Yesu? Karibu katika somo hili kujifunza kuhusu haya na mengine pia.
Mafundisho haya yanaendana na masomo yanayopatikana katika Kozi ya Maji ya Uzima inayoitwa Madaraja ya Kumfikia Mungu. Kwa maelezo zaidi kuhusiana na masomo haya au kujiunga na kozi wasiliana nasi kupitia
Barua pepe: neno@majiyauzima.com
Simu: +255754 490 549 / +255694 298 395 / +255719 275 767