Kwa nini Yesu alikuja duniani? Katika Mat 1:21 Biblia inasema kwamba alikuja kuwaokoa watu wake na dhambi zao. Kama ni hivyo tukiendelea katika dhambi lengo la Kristo halijatimia. Yesu alitufananisha na chumvi. Mat 5:13, Luk 14:34-35 Wakristo wasioweza kuishi katika ushindi ni kama chumvi iliyoharibika. Hawana kazi yoyote ila kutupwa nje. Mbaya zaidi ni kwamba tusipoishi katika ushindi bali tu watumwa wa dhambi tuko chini ya kiongozi yupi Shetani au Yesu? Bila shaka ni Shetani. Mungu ashukuriwe kwamba hatupaswi kuishi katika dhambi maana anaweza kuwaokoa kabisa wao wamjiao Ebr 7:25. Katika somo hili Ndugu Jeff anahimiza tuishi maisha yaliyobadilika kwa nguvu za Mungu. Mafundisho haya yanaendana na masomo yanayopatikana katika Kozi ya Maji ya Uzima inayoitwa Madaraja ya Kumfikia Mungu. Kwa maelezo zaidi kuhusiana na masomo haya au kujiunga na kozi wasiliana nasi kupitia
Barua pepe: neno@majiyauzima.com
Simu: +255754 490 549 / +255694 298 395 / +255719 275 767