19 Hatua ya Kwanza Somo 18-19; Yesu, Bwana Aliyefufuka

11 Oktoba, 2024

Kitabu: Yohana

Bible Passage: Yohana 19-20

Katika somo hili ndugu Jeff anapitia sura zote ya Injili ya Yohana na kukumbusha japo kwa maneno machache habari zinazopatikana katika kila sura. Pia tunajifunza katika sura ya 19 kwamba ilimpasa Yesu kujitoa kama mwana-kondoo wa kuchinjwa ili tuokolewe pamoja na kuleta Agano Jipya. Halafu katika sura ya 20 tunaona kwa ufupi maana ya kukutana kama kanisa siku ya Jumapili na mfano wa Mariamu Magdalena akimngojea Bwana wake kwa shauku.

Mafundisho haya yanaendana na masomo yanayopatikana katika Kozi ya Maji ya Uzima inayoitwa Hatua ya Kwanza.

Kwa maelezo zaidi kuhusiana na masomo haya au kujiunga na kozi wasiliana nasi kupitia

Barua pepe: neno@majiyauzima.com

Simu: +255754 490 549 / +255694 298 395 /+255719 275 767