14 Hatua ya Kwanza Somo 13-14; Yesu, Njia

20 Septemba, 2024

Kitabu: Yohana

Bible Passage: Yohana 13-14

Yesu alitufundisha kwamba tupendane. Injili ya Yohana 13:34 Amri mpya nawapa, Mpendane. Kama vile nilivyowapenda ninyi, nanyi mpendane vivyo hivyo. Kwa hiyo kama wafuasi wake Yesu tuwe mifano mizuri ya kupendana. Pia katika Sura hiyo Yesu alitufundisha kwamba kiongozi anapaswa kuwa mtumishi au anayetumika. Tusidhani kwa kuwa tuna nafasi kama kiongozi tuanze kujivuna na kuwatumikisha wengine. Si mfano wa Yesu. Pamoja na hivyo katika sura ya 14 Yesu anatuambia kwamba tukimpenda tutazishika amri zake. Tusidhani kwamba Yesu atatuombea Roho Mtakatifu kwa Baba kama hatujamheshimu na kushika amri zake. Ungana na Ndugu Jeff kujifunza haya na mengine pia.

Mafundisho haya yanaendana na masomo yanayopatikana katika Kozi ya Maji ya Uzima inayoitwa Hatua ya Kwanza.
Kwa maelezo zaidi kuhusiana na masomo haya au kujiunga na kozi wasiliana nasi kupitia
Barua pepe: neno@majiyauzima.com
Simu: +255754 490 549 / +255694 298 395 /+255719 275 767