13 Hatua ya Kwanza Somo 13-14: Yesu, Bwana – Mtumishi

20 Septemba, 2024

Kitabu: Yohana

Bible Passage: Yohana 13-14

Katika video hii kaka Mathayo anatuonyesha jinsi Yesu ndiye: BWANA – MTUMWA kama tunavyosoma katika Injili ya Yohana 13:13-14. Yesu alituonyesha kwamba kiongozi anatakiwa kuwa mtumwa kwa wafuasi wake. ALIYESALITIWA Yoh 13:21 Mmojawapo wa wanafunzi wake Yesu ndiye aliyemsaliti. Yesu alimwonesha Yuda upendo na heshima yote ingawa alikuwa tayari kumtendea vibaya. BWANA HARUSI Yoh 14:3 Yesu kama Bwana harusi anaenda kutuandalia makao ili tuishi pamoja milele. NJIA na UKWELI na UZIMA Yoh 14:6 Yesu ndiye jibu letu kwa mahitaji yetu yote, Yesu ndiye Ukweli kwake yeye tunapata kuelewa vyema ulimwengu ulivyo, Yesu ndiye uzima wetu bila yeye tumekufa bila tumaini. MSAIDIZI Yoh 14:16-17 Yesu anatuambia kwamba wanafunzi wake waliweza kumjua Msaidizi kupitia kwake maana yeye ndiye Msaidizi lakini atatutuma Msaidizi mwingine ili tusiwe watoto yatima.

Mafundisho haya yanaendana na masomo yanayopatikana katika Kozi ya Maji ya Uzima inayoitwa Hatua ya Kwanza.
Kwa maelezo zaidi kuhusiana na masomo haya au kujiunga na kozi wasiliana nasi kupitia
Barua pepe: neno@majiyauzima.com
Simu: +255754 490 549 / +255694 298 395 /+255719 275 767