Katika sura ya 11 ya Injili ya Yohana tunasoma habari za Yesu kumfufua Lazaro. Ndugu Jeff anaelezea jinsi sisi pia tulikuwa wafu lakini tumefufuliwa na Yesu kuishi kwa utukufu wake Mungu. Pia tunajifunza umuhimu wa kukiri Yesu na kuwa na ujasiri badala ya kumwonea Yesu haya. Ili Yesu naye asituone sisi haya. Yesu pia alizungumzia habari ya chembe ya ngano kupandwa na kufa ili izae. Kwa hiyo na sisi pia kama tutazaa lazima tutoe maisha yetu yote. Tusibakishe kitu.
Mafundisho haya yanaendana na masomo yanayopatikana katika Kozi ya Maji ya Uzima inayoitwa Hatua ya Kwanza.
Kwa maelezo zaidi kuhusiana na masomo haya au kujiunga na kozi wasiliana nasi kupitia
Barua pepe: neno@majiyauzima.com
Simu: +255754 490 549 / +255694 298 395 /+255719 275 767