Umewahi kuwa na maswali juu ya Biblia?
Biblia inasema katika 2 Tim 3:16 Kila andiko, lenye pumzi ya Mungu, lafaa kwa mafundisho, na kwa kuwaonya watu makosa yao, na kwa kuwaongoza, na kwa kuwaadibisha katika haki;
Halafu katika 2 Kor 3:6 Naye ndiye aliyetutosheleza kuwa wahudumu wa agano jipya; si wa andiko, bali wa roho; kwa maana andiko huua, bali roho huhuisha.
Kwa hiyo inamaana gani kuwa na maandiko haya yanayoonekana kuwa vitu viwili tofauti.
Katika video hii Mchungaji Justin anajitahidi kujibu maswali magumu ya namna hiyo.
Mafundisho haya yanaendana na masomo yanayopatikana katika Kozi ya Maji ya Uzima inayoitwa Madaraja ya Kumfikia Mungu. Kwa maelezo zaidi kuhusiana na masomo haya au kujiunga na kozi wasiliana nasi kupitia
Barua pepe: neno@majiyauzima.com
Simu: +255754 490 549 / +255694 298 395 / +255719 275 767