Tiba la dhambi ni Nani? Kusudi la Yesu kuja ulimwenguni lilikuwa nini?
Tofauti kati ya mtu aliyepotea na aliyeokolewa ni zipi? Karibu katika somo hili pamoja na ndugu Jeff. Utaweza kujifunza ni kwa sababu gani dhambi inakuwa na madhara makubwa halafu pia katika Hes 21:4-9 tunajifunza habari za Nyoka wa Shaba na jinsi tiba la dhambi linaweza kuwa tofauti sana na fikra zetu za kibinadamu.
Mafundisho haya yanaendana na masomo yanayopatikana katika Kozi ya Maji ya Uzima inayoitwa Madaraja ya Kumfikia Mungu. Kwa maelezo zaidi kuhusiana na masomo haya au kujiunga na kozi wasiliana nasi kupitia
Barua pepe: neno@majiyauzima.com
Simu: +255754 490 549 / +255694 298 395 / +255719 275 767