1.3 Miongozo ya Familia Katika Biblia; Familia (Kujenga Familia za Kikristo)

25 Julai, 2026

Kitabu: Waefeso

Bible Passage: Waefeso 5:25

Katika somo letu hili Kaka Mikaeli anaendeleza masomo ya familia, lakini katika somo hili alijikita zaidi juu ya ile miongozo iliyowekwa na MUNGU kutoka kwenye Biblia na ambayo familia zinapaswa kuifuata ili ziwe za kumpendeza MUNGU na jamii iliyowazunguka.
Ametufunza mengi katika somo hili nini mwanaume afanye kwa mkewe na nini mwanamke afanye kwa mumewe, hivyo alieleza kwa kina miongozo muuhimu ikiwemo upendo, kuheshimiana, kufanya mambo kwa utaratibu mzuri, nidhamu na kuwa watii kwa kila mmoja katika familia.
Na mwishowe alitukumbusha kuwa kila miongozo lazima iwe na kiongozi na akatuambia ni neno lipi MUNGU anatukumbusha kutoka katika Biblia hasa wanaume ambao ndiyo viongozi wa familia.
‘Enyi waume, wapendeni wake zenu, kama Kristo naye alivyolipenda kanisa, akajitoa kwa ajili yake'(Waefeso 5:25)

Mafundisho haya yanaendana na masomo yanayopatikana katika Kozi ya Maji ya Uzima inayoitwa Kujenga Familia za Kikristo. Kwa maelezo zaidi kuhusiana na masomo haya au kujiunga na kozi wasiliana nasi kupitia
Barua pepe: neno@majiyauzima.com
Simu: +255754 490 549 / +255694 298 395 / +255719 275 767
Tovuti: https://majiyauzima.com/