2.2 Malengo ya Uchumba; (Kujenga Familia za Kikristo)

6 Agosti, 2026

Mada: Familia, Uchumba

Kitabu: Mithali

Bible Passage: Mithali 16:17

Katika somo hili ndugu Jeff ametueleza kwa kina kuhusu malengo na sio malengo tu bali yale yanayompendeza Mungu na yanafikika kwa njia ya utakatifu, hasa akijikita zaidi katika eneo la uchumba.

Na akikiri wazi kuwa uchumba usio na malengo ni sawa na bure pia ni mtego hatari sana ambao unaweza kuwapelekea wawili hao kuangukia dhambini na hata kujinajisi.

Katika somo hili amezungumza mengi ya kushauri , kufuata na ya kuzingatia wakati wa uchumba kwani anaamini bila malengo katika uchumba ni sawa na kupotelea katika msitu mkubwa pasipokuwa na ramani… lakini katika yote hayo alisisitiza zaidi kuwa kwenye uchumba lengo lolote lile ni lazima lianze na MUNGU.. NDIYO MENGINE YAFUATIE.

Na akitukumbusha kuwa malengo yasiishie kwenye maneno tu bali kwa vitendo kama Suleimani asemavyo katika Biblia;(Mithali 16:17) Njia kuu ya mwenye haki ni kujitenga na uovu; Yeye ashikaye njia yake huihifadhi nafsi yake.

Mafundisho haya yanaendana na masomo yanayopatikana katika Kozi ya Maji ya Uzima inayoitwa Kujenga Familia za Kikristo. Kwa maelezo zaidi kuhusiana na masomo haya au kujiunga na kozi wasiliana nasi kupitia
Barua pepe: neno@majiyauzima.com
Simu: +255754 490 549 / +255694 298 395 / +255719 275 767
Tovuti: https://majiyauzima.com/