Katika soma hili mchungaji Tim ameelezea zaidi kuhusu jukumu katika muktadha wa ndoa na familia hasa zaidi akieleza jukumu la mume au baba katika familia.
nikweli tunaishi katika karne ambayo watu wamekua wakikimbia majukumu yao na kupelekea matokeo ya mitazamo hasi na mambo yasiyopendeza machoni pa MUNGU.
Aliweza kuzungumza mambo mengi ambayo ni nyenzo na muhimu kwa mwanaume kuyatambua kama majukumu yake ya lazima katika ndoa na aamini kwamba hakuna mtu mwingine yeyote atakayeyatimiza isipokua yeye kwanza. Na mambo ya msingi aliyoyaelezea kwa kina zaidi katika somo hili ni haya matatu KUPENDA, KUONGOZA na KUKIMU MAHITAJI, na kila moja ya hilo alikua akionesha wazi kwa mifano ya MUNGU kutoka katika Biblia.
KUPENDA; Njoni kwangu, ninyi nyote msumbukao na wenye kulemewa na mizigo, nami nitawapumzisha (Mathayo 11:28).
KUONGOZA; Lakini nataka mjue ya kuwa kichwa cha kila mwanamume ni Kristo…. (1 Wakorintho 11:3).
KUKIMU MAHITAJI; Nalikuwa kijana nami sasa ni mzee, lakini sijamwona mwenye haki ameachwa wala uzao wake ukiomba chakula (Zaburi 37:25)
Mafundisho haya yanaendana na masomo yanayopatikana katika Kozi ya Maji ya Uzima inayoitwa Kujenga Familia za Kikristo. Kwa maelezo zaidi kuhusiana na masomo haya au kujiunga na kozi wasiliana nasi kupitia
Barua pepe: neno@majiyauzima.com
Simu: +255754 490 549 / +255694 298 395 / +255719 275 767
Tovuti: https://majiyauzima.com/