9b Kukua Kikristo; (Tufanye Nini Tukue?) Madaraja ya Kumfikia Mungu

31 Mei, 2025

Bible Passage: 2 Pet 1:5-8

Mtu anayetaka kuwa fiti na mwenye nguvu anatakiwa afanye mazoezi. Tunapomfuata Kristo kuna mazoezi yanayoweza kutusaidia kukua na kuwa wenye nguvu kiroho. Ukisoma katika 2 Pet 1:5-8 utakuta mazoezi yanayomfaa kila mkristo. Tuwe na Imani, Wema, Maarifa, Kiasi, Subira, Utauwa, Upendano wa Ndugu, na Upendo. Tuwe nayo na kujaa tele. Tufanyeje ili matunda hayo yaonekane katika maisha yetu? Kaka Jason anatuonyesha namna ambavyo shida na dhiki zinaweza kutusaidia kukua zaidi.

Wakati mwingine ugonjwa unaweza kusababisha mtu asikue. Katika maisha ya kiroha pia tunakuta vikwazo ambavyo vinaweza kuwa kama magonjwa kwa wafuasi wa Kristo. Kama vile Wachungaji wasiojali, Kujikusanyia mali na Mapokeo ya mababu. Kristo anataka ukuwe uwe mkamilifu. Je! Uko tayari?

Mafundisho haya yanaendana na masomo yanayopatikana katika Kozi ya Maji ya Uzima inayoitwa Madaraja ya Kumfikia Mungu. Kwa maelezo zaidi kuhusiana na masomo haya au kujiunga na kozi wasiliana nasi kupitia

Barua pepe: neno@majiyauzima.com

Simu: +255754 490 549 / +255694 298 395 / +255719 275 767