9.1 Msalaba Una Maana Gani? Maswali na Majibu (Madaraja ya Kumfikia Mungu)

Bible Passage: Mat 16:24

Wengine wanavaa msalaba shingoni. Wakifanya hivyo wanatimiza maneno ya Yesu katika Mat 16:24? ( “Mtu yeyote akitaka kunifuata, na ajikane mwenyewe, ajitwike msalaba wake, anifuate.”) Au Yesu alimaanisha nini? Katika kipindi hiki Ndugu Jason akishirikiana na wengine aliweza kujibu maswali kama haya pamoja na kugusa kwenye mada ya Wanawake kuwa viongozi katika Kanisa.

Mafundisho haya yanaendana na masomo yanayopatikana katika Kozi ya Maji ya Uzima inayoitwa Madaraja ya Kumfikia Mungu. Kwa maelezo zaidi kuhusiana na masomo haya au kujiunga na kozi wasiliana nasi kupitia

Barua pepe: neno@majiyauzima.com

Simu: +255754 490 549 / +255694 298 395 / +255719 275 767