3.1 Kuzoea Mazingira Mapya; Mume na Mke (Kujenga Familia za Kikristo)

17 Julai, 2026

Mada: Familia, Ndoa

Kitabu: Mwanzo

Bible Passage: Mwanzo 2:24

Jizoeze na Mazingira. Ndio lilikuwa somo la kwanza la Mchungaji Tim , ambaye yeye anafundisha mada ya mke na mume , na kwa bahati nzuri ni mtu aliyekomaa katika ndoa ya zaidi ya miaka ishirini, na katika somo hili ameweza kuelezea uzoefu wake huo na kukiri kwamba hali haziwezi kua sawa kila siku.

Hii ni picha ambayo mchungaji Tim alitaka kijana awe nayo kichwani na aelewe ndiyo maana ya kuyazoea mazingira kwani mambo mengi ni mageni; Kuna tofauti kubwa sana. Jana nilikuwa rafiki wa kiume; leo mimi ni mume. Jana kulikuwa na uwezekano anyakuliwe na mwanamume mwingine; lakini sasa ni wangu. Jana mtazamo wangu ulikuwa wa kiume tu; lakini leo nastahili kuzingatia mambo kwa mtazamo wa kike pia. Jana haikuwa halali kumpapasa kimapenzi; lakini leo uhusiano wa kupapasana unaheshimika. Jana nilikuwa tu na jukumu kwangu binafsi; lakini leo nina jukumu kwetu sote wawili. Jana nilimwona akiwa amestaarabika; leo namwona katika hali yake ya kawaida. Jana ningeweza kumficha tabia zangu mbaya; leo itakuwa vigumu kuzificha. Jana niliishi katika ndoto; leo ndoto yangu imetimia. Jana sikuwa nimeoa/olewa; leo nina mke/mume. Hii ni tofauti kubwa sana.

Na alieza hayo yote yanatokea siyo bahati mbaya kwani ulikua ni mpango wa MUNGU tangu kuumbwba ulimwengu ya kwamba:(“Kwa hiyo mwanamume atamwacha baba yake na mama yake, naye ataambatana na mkewe; nao watakuwa mwili mmoja.) Mwanzo 2:24”

Mafundisho haya yanaendana na masomo yanayopatikana katika Kozi ya Maji ya Uzima inayoitwa Kujenga Familia za Kikristo. Kwa maelezo zaidi kuhusiana na masomo haya au kujiunga na kozi wasiliana nasi kupitia
Barua pepe: neno@majiyauzima.com
Simu: +255754 490 549 / +255694 298 395 / +255719 275 767
Tovuti: https://majiyauzima.com/