2.1 Matayarisho ya Uchumba; (Kujenga Familia za Kikristo)

17 Julai, 2026

Mada: Familia, Uchumba

Kitabu: Mithali

Bible Passage: Mithali 14:15

Video hii tunajikuta katika mwanzo wa masomo haya yanayohusiana na uchumba ambayo Ndugu Jeff atakua akifundisha. Yeye katika somo hili kajikita zaidi kwenye matayrisho sahihi ya uchumba ambayo yatapelekea ndoa bora.

Ametufundisha mambo mengi katika somo hili ikiwemo mambo muhimu ambayo mtu kabla ya kuanza safari hii anatakiwa kuyajua kama kuelewa ndoa na kuujua upendo, pamoja na matayarisho ya mtu binafsi , ambapo katika kipengele hicho alieleza kwa kina sana mambo muhimu na yanayopaswa kuzingatiwa kabla ya chochote.

Pia alitukumbusha nini Suleimani anatufundisha kutoka katika Biblia juu ya maamuzi…: (Mithali 14:15) Mjinga huamini kila neno; Bali mwenye busara huangalia sana aendavyo.

Mwishowe kulikuwa na mjadala na maswali kama yafuatayo: Katika kuanzisha familia nani anakuwa miliki ya mali?

Mafundisho haya yanaendana na masomo yanayopatikana katika Kozi ya Maji ya Uzima inayoitwa Kujenga Familia za Kikristo. Kwa maelezo zaidi kuhusiana na masomo haya au kujiunga na kozi wasiliana nasi kupitia
Barua pepe: neno@majiyauzima.com
Simu: +255754 490 549 / +255694 298 395 / +255719 275 767
Tovuti: https://majiyauzima.com/