Misingi, kama tunavyofahamu kila tunachokiona kimesimama lazima kitakua na msingi wake kuanzia chini. Yaweza kua kimesimama imara au hakiko imara na inaeleweka kwamba matokeo ya uimara wake yanasababishwa na msingi wake kwa ujumla.
Katika masomo yetu haya ya nyumba hasa katika somo hili Kaka Mikaeli ameweza kutufundisha zaidi kuhusu misingi akielekeza na kutilia mkazo zaidi katika kuundwa na kujengwa kwa misingi ya familia iliyo bora.
Lengo la Mungu lilikua ni bora na jema toka mwanzo wa kuumbwa ulimwengu na hata sasa kwamba ni liazima mwanaume aachane na wazazi wake na kwenda kuambatana na mkewe na wawe kitu kimoja (Mwanzo 2:24)
lakini kutokana na mazoea yetu sisi kama binadamu inatupelekea kuishi nje ya utaratibu wa mungu na mwishowe kuwa na familia sizizokua na matokeo bora kwa sababu ya misingi mibovu iliyoundwa toka mwanzo na wazazi wa hiyo familia’
ndio maana katika maisha yetu ya sasa tunaona mambo ya taraka , watu kuachana na uyu kwenda kuolewa na huyu na mengine pia mengi katufundisha mchungaji mikeli katika somo hili lakini hakatukumbusha mamlaka aliyo nayo mumngu tuu juu ya ndoa na hayupo mwanadamu mwenye hayo mamlaka hapa duniani.
Basi aliowaunganisha mungu mwanadamu asiwatenganishe (Mathayo 19:6) sio padri , sio shehe, sio hakimu, sio mchungaji wala mtu yeyote yule ambaye jamii inadhani hana haki ya kulifanya hilo bali ni MUNGU pekee.
Mafundisho haya yanaendana na masomo yanayopatikana katika Kozi ya Maji ya Uzima inayoitwa Kujenga Familia za Kikristo. Kwa maelezo zaidi kuhusiana na masomo haya au kujiunga na kozi wasiliana nasi kupitia
Barua pepe: neno@majiyauzima.com
Simu: +255754 490 549 / +255694 298 395 / +255719 275 767
Tovuti: https://majiyauzima.com/
