1.1 Mwanzo na Uendelezaji wa Familia; (Kujenga Familia za Kikristo)

17 Julai, 2026

Mada: Familia

Kitabu: Mwanzo

Bible Passage: Mwanzo 2:18-22

Familia, kama ilivyozoeleka katika tafsiri nyingi kuhusu familia hua zinakubaliana kwamba familia ni muunganiko wa baba, mama, na watoto hii ndiyo familia kuu japo zipo aina mabali mbali za familia.

Katika somo hili kaka Mikaeli naye analitambua hilo na ameweza kutufundisha ni namna gani tunaweza kuanzisha hiyo familia na namna nzuri ya kuweza kuiendeleza katika njia inayompendeza Mungu na wanadamu.

Ni kweli kila jambo lina mwanzo wake lakini ukweli usiopingika ni kwamba hatuwezi kua na mwanzo wa familia pasipo kua na jinsia mbili yaani ya kike na ya kiume apo ndipo tunaweza kuanza safari ya kujenga familia.

Na katika somo hili kaka Mikaeli ametukumbusha na kutufundisha kwamba hili jambo halipo kwa bahati mbaya ni makusudi yake Mungu muumba ambaye tangu mwanzo wa kuumba ulimwengu alimwumba mwanaume na baadae akamwumba mwanamke na apo ndipo vilipoanza vizazi vyote mpaka hii leo tupo mimi na wewe lakini chanzo alikua baba yetu Adamu na mama yetu Eva:( Mwanzo 2:18-22)

Pamoja na somo mwishoni kuliibuka maswali. Kama vile utanyaje ikiwa mwenza wako hakupendi? Ni kwa hali gani utaweza kurejesha upendo katika ndoa yako?

Mafundisho haya yanaendana na masomo yanayopatikana katika Kozi ya Maji ya Uzima inayoitwa Kujenga Familia za Kikristo. Kwa maelezo zaidi kuhusiana na masomo haya au kujiunga na kozi wasiliana nasi kupitia
Barua pepe: neno@majiyauzima.com
Simu: +255754 490 549 / +255694 298 395 / +255719 275 767
Tovuti: https://majiyauzima.com/