40 Mwana-Kondoo Yuko Wapi? Uko Tayari Kuwa Sadaka Mbele za Mungu? (Nyayo za Kristo)

Bible Passage: Warumi 12:1

Mwana Kondoo (mnyama aliye andaliwa kwa ajili ya sadaka) hapo zamani watu wa Mungu walitumia mnyama mkamilifu kwa ajili ya kumtolea sadaka Mungu na mara nyingi ilikua ni sadaka ya kuteketezwa.
Katika somo hili Mch Korosso ameweza kutufunza sisi wakristo hasa kwa kuzingatia maisha ya baba yetu Abrahamu na namna Mungu alimuhitaji amtoe mwanawe wa pekee kama sadaka ya kuteketezwa kwa moto, na wala hakubisha yeye na mwanae pia alikua tayari kwa hilo.
Na ameweza kutueleza kwamba ipo madhabau ya Mungu ambayo haijulikani na wa watu hawaitilii maanani nayo ni miili yetu na maisha yetu. Hivyo ametusihi sisi wakristo kwamba tunapaswa kujiweka wakifu kwa Mungu wetu kikamilifu bila makando kando yaani, kuikabidhi miili yetu, akili zetu, roho zetu, mali zetu na kujisalimisha kwa Mungu wetu na hiyo ndio itakua kama sadaka ya Abrahamu( yaani tuwe wanakondoo kwake Mungu) “Basi, ndugu zangu, nawasihi, kwa huruma zake Mungu, itoeni miili yenu iwe dhabihu iliyo hai, takatifu, ya kumpendeza Mungu, ndiyo ibada yenu yenye maana.” (Warumi 12:1.) Na mishowe iliimbwa tenzi ya rohoni namba 49. Ikiwa ni sehemu ya kulikubali hili la kujiweka chini ya Mungu na kuhitimisha mafunzo yetu.
Mafundisho haya yanaendana na masomo yanayopatikana katika Kozi ya Maji ya Uzima inayoitwa Nyayo za Kristo. Kwa maelezo zaidi kuhusiana na masomo haya au kujiunga na kozi wasiliana nasi kupitia
Barua pepe: neno@majiyauzima.com
Simu: +255754 490 549 / +255694 298 395 / +255719 275 767
Tovuti: https://majiyauzima.com/