39 Kristo na Madeni; Je, Deni Ndio Jambo Jema?

21 Aprili, 2026

Kitabu: Mithali

Bible Passage: Mithali 22:7

Deni ni nini? huu ni wajibu wa kifedha au mali ambao mtu, nchi au taasisi inadaiwa kurudisha kwa mwingine, baada ya kukopa au kupewa kitu kwa makubaliano ya kurejesha.japo ipo mijadala ambayo watu wanajaribu kutofautisha kati ya deni na mkopo. Katika somo letu, kristo na madeni ndugu jeff anakubaliana kabisa na maana hii na anataka sisi kama wakrito tufanye nini katika suala la madeni. Kwanza anakubali kwamba katika uharisia wa maisha yetu ya kila siku sisi kama binadamu upo uwezokano mkubwa wa kujikuta katika madeni na sio ya kifedha tuu yapo ya ki hali na hisia kwani “haadi ni deni pia”.
Hivyo katika somo hili ndugu jeff ameweza kutumia mifano na maandiko matakatifu katika kutufundisha ni nini yatupasa kufanya sisi tulio waamini katika kristo ili kuweza kushughulikia madeni pasipo kumkwaza mungu wala kutenda dhambi kwa sababu ya madeni. Na mwisho aliweza kutusihi sisi wakristo kwa namna yoyote hile na kwa bidii, tujitahidi kuepukana na hali hii ya kuwa katika madeni. kwani maandiko matakatifu yanasema ” Naye akopaye ni mtumwa wake akopeshaye”. (Mithali 22:7)
Mafundisho haya yanaendana na masomo yanayopatikana katika Kozi ya Maji ya Uzima inayoitwa Nyayo za Kristo. Kwa maelezo zaidi kuhusiana na masomo haya au kujiunga na kozi wasiliana nasi kupitia
Barua pepe: neno@majiyauzima.com
Simu: +255754 490 549 / +255694 298 395 / +255719 275 767
Tovuti: https://majiyauzima.com/