38 Kristo na Kazi; Kazi ni Baraka au Laana? (Nyayo za Kristo)

14 Aprili, 2026

Mada: Kazi

Kitabu: 2 Wathesalonike

Katika video hii Mwalimu Smith anatufundisha umuhimu wa kazi katika maisha ya waamini. Anatuhimiza kuwatafakari mchwa ambao wao ni viumbe wenye umbo dogo sana lakini wanalitambua hili na kulifanya kwa umoja pasi na msimamizi wala mwamuzi.
Katika somo hili ameweza pia kusisitiza umuhimu wa kufanya kazi na faida zake na kukemea pia uvivu na madhara yake.
Na kwa kutambua umuhimu wa kufanya kazi aliona ni vyema kutuainishia kazi ambazo tunapaswa kuzifanya na ambazo hatupaswi kuzifanya sisi tulio waamini katika Kristo, ili kwamba tusiingie majaribuni kwa kutenda yasiyofaa katika kulitimiza jukumu hili ambalo kimsingi lipo tangia kuumbwa kwa ulimwengu huu na aliagizwa baba yetu Adamu alitimize.
Na alitusihi kwamba wapo ambao hawawezi kufanya kazi kwa sababu zilizo nje ya uwezo wao , hao wanahitaji msaada wetu . Na ametuonesha Biblia inasema yapi kwa wanaolifuata hilo agizo la kufanya kazi “Basi tunawaagiza hao, na kuwaonya katika Bwana Yesu Kristo, wafanye kazi kwa utulivu na kula chakula chao wenyewe”. (2 Wathesalonike 3:12)

Mafundisho haya yanaendana na masomo yanayopatikana katika Kozi ya Maji ya Uzima inayoitwa Nyayo za Kristo. Kwa maelezo zaidi kuhusiana na masomo haya au kujiunga na kozi wasiliana nasi kupitia

Barua pepe: neno@majiyauzima.com
Simu: +255754 490 549 / +255694 298 395 / +255719 275 767
Tovuti: majiyauzima.com