28 Kristo na Kanuni Yake ya Upendo; Unafuata Kanuni Hiyo? (Nyayo za Kristo)

2 Oktoba, 2025

Kitabu: 1 Korintho, Mathayo

Tukisoma katika 1 Kor 13:4-7 Mungu ameweza kutuonesha sifa nyingi za upendo na jinsi unavyo jidhihilisha katika matendo. Na katika somo hili ndugu Jeff anakubaliana na sifa hizo za upendo lakini ameweza kuzungumzia zaidi ni jinsi gani tunaweza kuzitumia kanuni za upendo katika kuudumisha upendo miongoni mwetu kama ndugu wa kiroho.

Kwani sio kwamba tukipendana hatuwezi kutofautiana, sio kweli sisi ni binadamu tunaweza kutofautiana kwa mambo tofauti na hata kukoseana pia.

Hivyo katika somo hili ndugu Jeff amefundisha kanuni za kufuata pale ndugu anapokukosea na ambazo hautakiwi kuzifuata pale ambapo ndugu kakukosea na kutukumbusha maagizo matakatifu kutoka katika Biblia Mt 18:15 Na ndugu yako akikukosea, nenda ukamwonye, wewe na yeye peke yenu, akikusikia umempata nduguyo.

Mafundisho haya yanaendana na masomo yanayopatikana katika Kozi ya Maji ya Uzima inayoitwa Nyayo za Kristo. Kwa maelezo zaidi kuhusiana na masomo haya au kujiunga na kozi wasiliana nasi kupitia.

Barua pepe: neno@majiyauzima.com

Simu: +255754 490 549 / +255694 298 395 / +255719 275 767

Tovuti: majiyauzima.com