06 Kristo Dhidi ya Hasira; Kukasirika ni Dhambi? (Nyayo za Kristo)

7 Febuari, 2025

Kitabu: Efeso

Je! Hasira ni dhambi? Ukimkasirikia mnyama ni dhambi? Katika kitabu cha Waefeso tunasoma Muwe na hasira, ila msitende dhambi; jua lisichwe na uchungu wenu bado haujawatoka; wala msimpe Ibilisi nafasi. (Efe 4:26-27) Kuna utofauti gani kati ya hasira ya Mungu na hasira ya mwanadamu? Karibu katika somo hili. Kaka Tim anatufundisha mengi yanayohusiana na hasira. Hisia ambayo bila shaka sote tumewahi kuwa nayo. Umewahi kutenda jambo kwa hasira ambalo umelijutia baadaye? Tunawezaje kushinda hasira zetu? Utajifunza kuhusu hayo na mengine pia unaposikiliza video hii. Mungu akubariki.

Mafundisho haya yanaendana na masomo yanayopatikana katika Kozi ya Maji ya Uzima inayoitwa Nyayo za Kristo. Kwa maelezo zaidi kuhusiana na masomo haya au kujiunga na kozi wasiliana nasi kupitia

Barua pepe: neno@majiyauzima.com

Simu: +255754 490 549 / +255694 298 395 / +255719 275 767