4.4 Kuwalea Katika Adabu na Maonyo ya Bwana; (Kujenga Familia za Kikristo)

Katika somo hili mchungaji Korosso aliweza kuhitimisha masomo ya mfululizo wetu wa kuwalea watoto.
Aliweza kufundisha juu ya mambo yafuatayo;
1. Heshima
Wazazi wana wajibu wa kuwalea watoto katika kumcha, kumheshimu, na kumtii Mungu tangu wakiwa wadogo.
Mtumishi anatoa mfano wa Hana kwenye Bibilia (1 Samueli 1:27-28), aliyeomba mtoto na kuahidi kumtoa kwa Bwana.

2.Utiifu
Utiifu huleta baraka kwa mtoto na familia.
Mchungaji anatoa mfano wa Mfalme Sauli ambaye alionyesha utiifu wa nusu/pungufu kwa kutosikiliza maagizo yote ya Mungu, jambo lililopelekea kukataliwa kwake (1 Samueli 15)

3. Uadilifu
Watoto wafundishwe kusema ukweli na kuepuka uongo na udanganyifu.
Wazazi wanapaswa kuwaongoza na kuwachagulia watoto marafiki wema ili kuwalinda na tabia mbaya

4. Kazi
Watoto wafundishwe kufanya kazi kwa bidii na kujiepusha na uvivu tangu wakiwa wadogo (2 Wathesalonike 3:10)
Lengo la kufanya kazi ni kupata riziki halali na pia kupata uwezo wa kuwasaidia wengine wenye mahitaji kama wajane na yatima (Waefeso 4:28)

Mafundisho haya yanaendana na masomo yanayopatikana katika Kozi ya Maji ya Uzima inayoitwa Kujenga Familia za Kikristo. Kwa maelezo zaidi kuhusiana na masomo haya au kujiunga na kozi wasiliana nasi kupitia
Barua pepe: neno@majiyauzima.com
Simu: +255754 490 549 / +255694 298 395 / +255719 275 767
Tovuti: https://majiyauzima.com/