Katika somo hili mchungaji Tim ameelezea zaidi kuhusu jukumu katika muktadha wa ndoa na familia hasa zaidi akieleza jukumu la mke au mama katika familia.
Ni kweli tunaishi katika karne ambayo watu wamekua wakikimbia majukumu yao na kupelekea matokeo ya mitazamo hasi na mambo yasiyopendeza machoni pa MUNGU.
Kiukweli katika mpango wa MUNGU mwanaume bila mke hajakamilika bado ndiyo maana tunaona Adamu aliumbwa na sifa nyingi lakini bado MUNGU aliona si vyema awe peke yake akampatia msaidizi wa kufanana nae (Eva), kwa muktadha huu mchungaji Tim anakubali kuwa jukumu kubwa la mwanamke kwa mwanaume ni kuwa msaidizi ivyo alifundisha kuhusu , kumpenda mumeo, kumheshimu, kuwa mshauri, kuwa msaada kiroho na kimwili na mengi mazuri ambayo mwanamke anapasa kuyafanya kwa mumewe na akiamini mwanamke akiyafanya hayo vyema itapelekea hata watoto na watu kwenye familia kumuheshimu.
Na pia itakuwa ni baraka kwa mumewe pia, kwani Biblia inasema (Mithali 18:22) “Apataye mke apata kitu chema; Naye ajipatia kibali kwa BWANA.”
Mafundisho haya yanaendana na masomo yanayopatikana katika Kozi ya Maji ya Uzima inayoitwa Kujenga Familia za Kikristo. Kwa maelezo zaidi kuhusiana na masomo haya au kujiunga na kozi wasiliana nasi kupitia
Barua pepe: neno@majiyauzima.com
Simu: +255754 490 549 / +255694 298 395 / +255719 275 767
Tovuti: https://majiyauzima.com/