Katika somo hili Ndugu jeff amefundisha na kueleza kwa kina juu ya mashauri yaliyobora na yanayohitajika wakati wa uchumba, hivyo aliweza kufundisha mambo ya msingi yakufuata kama kutembeleana, kujua mnakutaniana wapi na kwa nini, kuepuka shida, kuwa wavumilivu, kutokua wachoyo na kutomfanyia mwenzako yale mambo ambayo wewe haupendi kufanyiwa.
Na alisisitiza kuwa uchumba ndiyo hatua ambayo watu huanza kujuana hivyo basi yapo mengi mageni hujitokeza na ni kawaida, lakini la muhimu alilolizingatia ni kwamba ni vyema kuyachunguza hayo mashaka yetu kama ni ya msingi au si ya msingi.
Pia alieleza kua uchumba siyo gereza, akimaanisha kwamba mnaweza mkapendana lakini kwa sababu zilizo nje ya uwezo wenu mkaona ni vyema kusitisha uchumba huo kwa utaratibu unaofaa. Akikiri kuwa hiyo ni sahihi lakini isijekuwa ndiyo mwanzo wa chuki au uadui baina yenu. Hapo itakua kinyume na mapenzi ya MUNGU; (Mathayo-22:37-39)
Mafundisho haya yanaendana na masomo yanayopatikana katika Kozi ya Maji ya Uzima inayoitwa Kujenga Familia za Kikristo. Kwa maelezo zaidi kuhusiana na masomo haya au kujiunga na kozi wasiliana nasi kupitia
Barua pepe: neno@majiyauzima.com
Simu: +255754 490 549 / +255694 298 395 / +255719 275 767
Tovuti: https://majiyauzima.com/