Katika somo hili ndugu Jeff alijikita zaidi kuhusu ushauri wa kufuata wakati wa uchumba, pia aliweza kufundisha mambo mengi sana ya muhimu na ya kuzingatia na pia yale ya kuyaepuka wakati wa uchumba na akiamini zaidi kuwa uchumba ndiyo hatua muhimu sana ya kujifunza kuhifadhi utakatifu.
Aliweza pia kufundisha nini cha kufanya na wapi pakupata ushauri sahihi, akikumbusha pia kuwa wazazi , familia , viongozi wa kiroho na watu walioko katika ndoa na wamekomaa hao ndiyo wanaweza kuwa na ushauri mzuri katika uchumba.
Pia alifundisha ni upi ni ushauri kwa kijana wa kiume na upi ni ushauri kwa kijana wa kike katika safari ya uchumba hili kufikia ndoa bora yenye kumpendeza MUNGU na jamii kwa ujumla.
Mafundisho haya yanaendana na masomo yanayopatikana katika Kozi ya Maji ya Uzima inayoitwa Kujenga Familia za Kikristo. Kwa maelezo zaidi kuhusiana na masomo haya au kujiunga na kozi wasiliana nasi kupitia
Barua pepe: neno@majiyauzima.com
Simu: +255754 490 549 / +255694 298 395 / +255719 275 767
Tovuti: https://majiyauzima.com/