Mungu hapendi kwamba tufanye makosa. Lakini ni nani ambaye hajakosea? Katika (1 Yohana 2:1) Tunasoma “Watoto wangu wadogo, nawaandikia haya ili kwamba msitende dhambi. Na kama mtu akitenda dhambi tunaye Mwombezi kwa Baba, Yesu Kristo mwenye haki,” Kwa hiyo kutenda dhambi haitakiwi lakini Yesu anatujua. Kwa hiyo ameweka utaratibu wa kufuata tukikosea. Ungana na kaka Smith kujifunza zaidi.
1. Ni lazima tutambue dhambi zetu.
2. Ni lazima kukiri dhambi zetu.
3. Ni lazima kuacha dhambi zetu.
4. Ni lazima kufanya marejesha kwa yule tuliyemkosea.
Mafundisho haya yanaendana na masomo yanayopatikana katika Kozi ya Maji ya Uzima inayoitwa Nyayo za Kristo. Kwa maelezo zaidi kuhusiana na masomo haya au kujiunga na kozi wasiliana nasi kupitia
Barua pepe: neno@majiyauzima.com
Simu: +255754 490 549 / +255694 298 395 / +255719 275 767