Katika 1 Kor 9:27 Paulo anasema kwamba anautesa mwili wake. Alimaanisha nini? Sisi je! Tunapaswa kutesa miili yetu? Karibu katika somo hili. Ndugu Jeff anafundisha umuhimu wa kutokuwa mvivu. Ni vigumu sana kwa Wakristo wengi kutenga muda kwa ajili ya Mungu. Je, umeridhika na maisha yako ya maombi? Je, unasoma Biblia kama unavyotakiwa? Mara nyingi umesema huna muda wa kuomba na kusoma Biblia, au unatoa visingizio vingine. Bali ukweli ni kwamba wewe ni mvivu. Au siyo? Hakika ni kweli! Unahitaji nidhamu binafsi. Unahitaji kumwomba Bwana Yesu akupatie hilo. Bila shaka, unapaswa kufanya sehemu yako. Unapaswa kuuwekea nidhamu mwili wako kila siku. Usijionee huruma kwa hili!
Mafundisho haya yanaendana na masomo yanayopatikana katika Kozi ya Maji ya Uzima inayoitwa Nyayo za Kristo. Kwa maelezo zaidi kuhusiana na masomo haya au kujiunga na kozi wasiliana nasi kupitia
Barua pepe: neno@majiyauzima.com
Simu: +255754 490 549 / +255694 298 395 / +255719 275 767