Tulio wengi tunaamini kwamba Hiari Hushinda Utumwa na Kutoa ni Moyo na Sio Utajiri. Katika somo hili ndugu Jeff ameweza kuyazungumzia haya yote kwa pamoja yaani kutoa kwa hiari na akizingatia mifano na maisha ya waliotutangulia kiimani yaani wafalme, mitume, na manabii ni nini walifanya walipokua wakilitenda jambo hilo.
Amekiri wazi kwamba kumekuwepo na baadhi ya watu ambao wao wemelifanya jambo hili kua kama deni au kitu cha lazima miongoni mwa waamini, wakati haitakiwi kuwa hivyo.
Na ni kwa sababu zipo sababu za kimsingi kabisa ambazo tukizifuata kwa moyo mkunjufu sisi kama wakristo , hakutakuwa na sababu ya kulazimishana au kuhimizana katika kujitoa kwa Mungu hiwe ni kihali au kimali.
Na ameweza kutueleza ni jinsi gani hasa Mungu wetu hupendezwa na sisi tunapomtolea kwa hiari na kwa moyo wa shukurani kwa kunukuu katika maandiko matakatifu.
“Kila mtu na atende kama alivyokusudia moyoni mwake, si kwa huzuni, wala si kwa lazima; maana Mungu humpenda yeye atoaye kwa moyo mkunjufu”. (2 Wakorintho 9:7)