Katika somo hili Mch. Korosso anatufundisha sisi wakristo ambao ni familia pia kutoka kwa baba yetu mmoja Mungu, ni namna gani tunatakiwa kuwa na utaratibu wa kufanya ibada nyumbani mwetu pamoja na wanafanilia ambao Mungu ametupatia kama vile watoto, mke au mume.
Ameeleza zaidi kwa mfano wa Ibrahimu namna alivyokua na huo utaratibu. Na kutusihi akina baba ambao ni vichwa katika hizo familia na akina mama ambao ni wasaidizi ni namna gani nzuri ya kuziendesha hizo ibada katika familia zetu na isiishie tu kuwa na ibada za kanisani.
Na kutukumbusha akina baba tunavyoagizwa na maandiko matakatifu, “Nanyi, akina baba, msiwachokoze watoto wenu; bali waleeni katika adabu na maagizo ya Bwana” (Waefeso 6:4)
Mafundisho haya yanaendana na masomo yanayopatikana katika Kozi ya Maji ya Uzima inayoitwa Nyayo za Kristo. Kwa maelezo zaidi kuhusiana na masomo haya au kujiunga na kozi wasiliana nasi kupitia.
Barua pepe: neno@majiyauzima.com
Simu: +255754 490 549 / +255694 298 395 / +255719 275 767
Tovuti: majiyauzima.com