Ndoa ni nini? kulingana na maandiko matakatifu ndoa ni wakati ambapo mwanaume ambaye hajaoa na mwanamke ambaye hajaolewa wanapoachana na wazazi wao na Mungu anawaunganisha kuwa kitu kimoja kupitia viapo kwenye tukio rasmi.
Katika somo hili ndugu Tim ameweza kutufundisha mambo mengi sana juu ya suala la ndoa, na kutufundisha makusudi ya mwenyezi Mungu kwa nini aliianzisha ndoa. Na kueleza namna watu sehemu mbali mbali wanavyofanya mizaha juu ya jambo hili tukufu machoni pa Mungu . Pia alitukumbusha sisi kama wakristo nini tunaagizwa na Biblia takatifu juu ya ndoa.
“Lakini kwa sababu ya zinaa kila mwanamume na awe na mke wake mwenywewe, na kila mwanamke na awe na mume wake mwenyewe” ( 1 Wakorintho 7:2)
Mafundisho haya yanaendana na masomo yanayopatikana katika Kozi ya Maji ya Uzima inayoitwa Nyayo za Kristo. Kwa maelezo zaidi kuhusiana na masomo haya au kujiunga na kozi wasiliana nasi kupitia.
Barua pepe: neno@majiyauzima.com
Simu: +255754 490 549 / +255694 298 395 / +255719 275 767
Tovuti: majiyauzima.com
 
				 
                                            

