30 Kristo na Uchumba; Ndoa Yenye Msingi Inaanzishwaje? (Nyayo za Kristo)

16 Oktoba, 2025

Mada: Uchumba

Kitabu: 1 Thes

Bible Passage: 1 Thes 4:3

Uchumba; kwa tafsiri ya tulio wengi hua tunafahamu ni ile hatua ya mwanzoni kabisa katika kuelekea safari ya ndoa baina ya binti na kijana kisha kua mume na mke. Katika somo hili kaka Smith anakiri kwamba katika Biblia hakuna sehemu ambayo imeandikwa au kutoa maelezo ya moja kwa moja kuwa ni nini kifanyike kuukamilisha uchumba. Hata katika dunia ya sasa ni ngumu kuupata muongozo wa moja kwa moja juu ya uchumba. naye anaamini huenda ni kwasababu ya kuwepo kwa tamaduni, mila, na desturi tofauti.
Hivyo katika somo hili ameweza kufundisha zaidi kuhusu ni yapi kama kijana anatakiwa kuyafuata kabla ya kuanza safari ya uchumba , pia ni yapi ambayo kama binti na kijana hawatakiwi kuyafanya wakiwa katika kipindi cha uchumba. Na ameeleza ni kwa namna gani vijana wengi huanza kujihusisha na mambo ya chumbani katika uchumba , kisha kukumbusha Biblia inatuambia nini katika hayo mambo. 1 The 4:3 Maana haya ndiyo mapenzi ya Mungu, kutakaswa kwenu, mwepukane na uasherati.

Mafundisho haya yanaendana na masomo yanayopatikana katika Kozi ya Maji ya Uzima inayoitwa Nyayo za Kristo. Kwa maelezo zaidi kuhusiana na masomo haya au kujiunga na kozi wasiliana nasi kupitia.

Barua pepe: neno@majiyauzima.com

Simu: +255754 490 549 / +255694 298 395 / +255719 275 767

Tovuti: majiyauzima.com