29 Kristo na Nidhamu Katika Ndugu: Tufanyeje Ndugu Yetu Akikosa? (Nyayo za Kristo)

Bible Passage: 1 Kor 5:7

Ikiwa ni katika mwendelezo wa masomo juu ya undugu, kaka Mikaeli ameweza kutufundisha ni taratibu zipi za kinidhamu ambazo tunatakiwa kuzifuata kama ndugu wa kiroho ili kuendelea kudumisha upendo , amani na kuhudumiana kama ndugu.

Katika somo hili kaka Mikaeli ameweza kufundisha taratibu nyingi za kufuatwa wakati pale ambapo ndugu yako kakukosea au kavunja baadhi ya taratibu mlizoziweka katika kanisa, ameeleza nyingi sana lakini katika zote hizo zinazingatia sana usiri, hekima, nidhamu na ushirikishwaji wa mashahidi. Na aliweza kutukumbusha umuhimu wa kuyafanya hayo miongoni mwetu kwa kutumia kifungu cha Biblia 1 Kor 5:7 Basi, jisafisheni, mkatoe ile chachu ya kale, mpate kuwa donge jipya, kama vile mlivyo hamkutiwa chachu.

Mafundisho haya yanaendana na masomo yanayopatikana katika Kozi ya Maji ya Uzima inayoitwa Nyayo za Kristo. Kwa maelezo zaidi kuhusiana na masomo haya au kujiunga na kozi wasiliana nasi kupitia.

Barua pepe: neno@majiyauzima.com

Simu: +255754 490 549 / +255694 298 395 / +255719 275 767

Tovuti: majiyauzima.com