Je! Ni sahihi Kanisa au viongozi kuamua au kuweka miongozo juu ya utaratibu sahihi katika uendeshaji wa shughuli za kikanisa, hata kama haziko wazi katika Biblia? Katika somo hili mchungaji Korosso ameweza kujibu vyema swali hili na pia ameweza kutufundisha juu ya mipaka na viwango ambavyo Kanisa linatakiwa kuzingatia katika jambo hili, na kurejea kwenye Biblia ni nini Mungu alituagiza katika hili Mt 18:18-19 Amini nawaambieni, yoyote mtakayoyafunga duniani yatakua yamefungwa mbinguni; na yoyote mtakayoyafungua duniani yatakua yamefunguliwa mbinguni, Tena nawaambia ya kwamba wawili wenu watakapo patana duniani katika jambo lolote watakaloliomba, watafanyiwa na Baba yangu aliye mbinguni.
Mafundisho haya yanaendana na masomo yanayopatikana katika Kozi ya Maji ya Uzima inayoitwa Nyayo za Kristo. Kwa maelezo zaidi kuhusiana na masomo haya au kujiunga na kozi wasiliana nasi kupitia
Barua pepe: neno@majiyauzima.com
Simu: +255754 490 549 / +255694 298 395 / +255719 275 767
Tovuti: majiyauzima.com
 
				 
                                            

