Huduma ni nini? Imezoeleka katika jamiii zetu kuwa huduma ni kitendo cha kumsaidia au kumtumikia mtu mwingine au kundi la watu kwa njia yoyote ile inayolenga mahitaji yao. Ni maana sahihi kabisa inayoendana na somo letu. Ndiyo maana Mchungaji Tim ameweza kutufafanulia zaidi juu ya huduma hasa kwa ndugu wa kiroho yaani (wakristo). Na aliweza kutueleza haijawa kwa bahati mbaya sisi kuwa ndugu wa kiroho yapo makusudi mengi ya mwenyenzi Mungu katika hili, ndio maana kuna vipawa mbali mbali miongoni mwetu ili kwamba kila mmoja awe sehemu ya huduma kwa mwingine katika kuyatimiza maagizo ya Mungu juu ya undugu. Na kwa kutumia maandiko ya Biblia aliweza kutuonesha ni maagizo gani Mungu katuachia katika jambo hilo Gal 6:10 kwa hiyo kadiri tupatavyo nafasi na tuwatendee watu wote mema; na hasa jamaa ya waminio.
Mafundisho haya yanaendana na masomo yanayopatikana katika Kozi ya Maji ya Uzima inayoitwa Nyayo za Kristo. Kwa maelezo zaidi kuhusiana na masomo haya au kujiunga na kozi wasiliana nasi kupitia
Barua pepe: neno@majiyauzima.com
Simu: +255754 490 549 / +255694 298 395 / +255719 275 767
Tovuti: majiyauzima.com
 
				 
                                            

