25 Kristo na Siku ya Bwana; Ina Umuhimu Gani? (Nyayo za Kristo)

10 Septemba, 2025

Mada: Sabato

Kitabu: Marko

Bible Passage: Mk 2:27

Siku ya Bwana ni ipi? kwa mujibu wa Biblia ni siku ya kwanza ya juma, ambayo katika imani ya wakristo iko na maana kubwa sana kwani ndiyo siku ambayo Yesu Kristo aliweza kufufuka na pia hata wanafunzi na waamini wa mwanzo walikua na desturi ya kukutana pamoja katika siku hiyo. Katika somo hili ndugu Smith ameweza kuturejesha nyuma kidogo katika agano la kale na kutuelezea nini maana ya sabato. Na hii ni kwa sababu ya kuwepo kwa waamini ambao wana misimamo mikali juu ya sabato na kuihusisha kama ndiyo siku ya Bwana.

Na aliweza kunukuu maelezo ya Yesu mwenyewe juu ya jambo hili kutoka katika Biblia Mk 2:27 akawaambia, na Sabato ilifanyika kwa ajili ya mwanadamu, si mwanadamu kwa ajili ya sabato.

Mafundisho haya yanaendana na masomo yanayopatikana katika Kozi ya Maji ya Uzima inayoitwa Nyayo za Kristo. Kwa maelezo zaidi kuhusiana na masomo haya au kujiunga na kozi wasiliana nasi kupitia.

Barua pepe: neno@majiyauzima.com

Simu: +255754 490 549 / +255694 298 395 / +255719 275 767

Tovuti: majiyauzima.com