Ibada ni nini? Ni hali au kitendo ambacho mtu ukitengea muda katika ratiba zake kwa ajili ya kuomba, kushukuru, kutukuza, kutoa sadaka na kutafakari juu ya kile ambacho yeye anaamini ndio kina mamlaka na nguvu zaidi yake katika maisha yake (MUNGU) Sasa kutokana na kuwepo kwa maana hiyo kumepelekea kuwa na ibada nyingi sana na miungu wengi pia.
Katika somo hili Mch Mtende ameweza kufundisha zaidi juu ya ibada katika ndugu wanaomuamini Mungu na kuzifuata Nyayo za Kristo, naye amekiri pia kuwa ipo miungu tofauti na baadhi kaweza kuishuhudia hivyo alitukumbusha kwa kurejea kwenye Biblia Zab 20:7 Hawa wanataja magari na hawa farasi, Lakini sisi tutalitaja jina la BWANA, Mungu wetu.
Mafundisho haya yanaendana na masomo yanayopatikana katika Kozi ya Maji ya Uzima inayoitwa Nyayo za Kristo. Kwa maelezo zaidi kuhusiana na masomo haya au kujiunga na kozi wasiliana nasi kupitia
Barua pepe: neno@majiyauzima.com
Simu: +255754 490 549 / +255694 298 395 / +255719 275 767
Tovuti: majiyauzima.com