22 Kristo na Taabu ya Mwanadamu; Kwa nini Tuna Matatizo Katika Maisha Yetu? (Nyayo za Kristo)

21 Agosti, 2025

Kitabu: Warumi

Bible Passage: Warumi 1:21

 Taabu juu ya Wanadamu: hili linamhusu kila mtu iwe unamwamini Kristo au humwanini. Ndugu January ameweza kutufunza mengi katika somo hili juu ya sababu ya hiyo taabu kuendelea kuwepo kwenye maisha yetu ingali kuwa mwenyezi Mungu ni mwenye upendo nasi. Alirejea katika Biblia kifungu cha Warumi 1:21 ” kwa sababu, walipomjua Mungu hawakumtukuza kama ndiye Mungu wala kumshukuru; bali walipotea katika uzushi wao, na mioyo yao yenye ujinga ikatiwa giza.” Kwa maana hiyo licha ya kuwa baba na mama yetu wa mwanzo (Adamu na Hawa ) kuasi pale bustanini na kuiacha laana hiyo, pia sisi kama wanadamu mwenendo na matendo yetu ya kila siku huenda ndiyo ikawa sababu kubwa ya kuwepo kwa taabu hizi katika maisha yetu ikiwa ni kama mshahara wa hayo. Pia alitufundisha ni jinsi gani ya kuwasaidia ambao wapo kwenye taabu ambazo zipo ndani ya uwezo wetu katika kuwasaidia.

Mafundisho haya yanaendana na masomo yanayopatikana katika Kozi ya Maji ya Uzima inayoitwa Nyayo za Kristo. Kwa maelezo zaidi kuhusiana na masomo haya au kujiunga na kozi wasiliana nasi kupitia

Barua pepe: neno@majiyauzima.com

Simu: +255754 490 549 / +255694 298 395 / +255719 275 767

Tovuti: majiyauzima.com