Unapozungumzia serikali na siasa unakua unagusa sehemu kuu na muhimu sana katika jamii au taifa. Mchungaji Korosso anatufundisha na kutukumbusha sisi kama wafuasi wa Kristo ni nini cha kufanya au ni namna gani ya kujihusisha na mambo hayo, kwani hayaepukiki katika maisha yetu ya kila siku. Hakuishia hapo aliweza kutuambia Mungu anatuagiza nini juu ya hao walio na mamlaka katika serikari na kwenye siasa 1Pet 2:13 “Tiini kila kiamriwacho na watu, kwa ajili ya Bwana; iwe ni mfalme, kama mwenye cheo kikubwa;” Pia katika Biblia tunaamini kila serikali iwe ya kidikteta au katili imewekwa na Mungu mwenyewe kwa makusudi ya ukuu wake. Hivyo alitusihi sisi kama wakristo tusiwe sehemu ya maandamano, vurugu, ghasia na uchochezi wa namna yeyote vile bali tuwe watii kwa mamlaka kama ni kodi tulipe, kwani jukumu letu sisi sio kujihusisha kwa kina na masuala hayo bali ni kuwaombea hao waliteuliwa na Mungu ili waweze kutuongoza katika hofu na haki yake Muumba.
Mafundisho haya yanaendana na masomo yanayopatikana katika Kozi ya Maji ya Uzima inayoitwa Nyayo za Kristo. Kwa maelezo zaidi kuhusiana na masomo haya au kujiunga na kozi wasiliana nasi kupitia
Barua pepe: neno@majiyauzima.com
Simu: +255754 490 549 / +255694 298 395 / +255719 275 767
Tovuti: majiyauzima.com