19 Kristo na Kiasi katika Mavazi; Kujipamba Inatakiwa? (Nyayo za Kristo)

31 Julai, 2025

Kitabu: 1 Petro

Mavazi ni nini? Tukichunguza tunakuta kua mavazi ni kwa ajili ya kustiri mwili au maungo ya mwanadamu. Imekua ni tofauti sana kwenye maisha ya sasa kutokana na kuwepo wa utandawazi kwa kiasi kikubwa hivyo kupelekea watu kukosa kiasi hata maadili katika uvaaji wa hayo mavazi (wao wanaita mitindo au fashion za kisasa). Kwa kulitambua hilo ndugu Mikaeli anatuelewesha kwa kina sisi kama wakiristo ni jinsi gani ya kuvaa au kua na kiasi juu ya mavazi kwani hili limekua tatizo kubwa hadi makanisani limekwisha kuingia. Alirejea katika 1Pet 3:3 “Kujipamba kwenu, kusiwe kujipamba kwa nje, yaani, kusuka nywele; na kujitia dhahabu na kuvalia mavazi;” Na si kwamba tusinunue mavazi La hasha! bali tuwe na mavazi yenye sitara na nadhifu, ili kwamba isifike wakati tukajipa thamani na utofauti na watu kwa sababu ya mitindo tuliyovaa au gharama za hayo mavazi na hata kuwa sababu ya mwingine kiingia katika jaribu la dhambi kutokana na mavazi yetu.

Mafundisho haya yanaendana na masomo yanayopatikana katika Kozi ya Maji ya Uzima inayoitwa Nyayo za Kristo. Kwa maelezo zaidi kuhusiana na masomo haya au kujiunga na kozi wasiliana nasi kupitia.

Barua pepe: neno@majiyauzima.com

Simu: +255754 490 549 / +255694 298 395 / +255719 275 767

Tovuti: majiyauzima.com