18 Kristo Dhidi ya Makanisa ya Uongo Yaliyopotea; Kanisa Lipi ni Kanisa la Kweli?

24 Julai, 2025

Kitabu: 1 Korintho, Efeso

Bible Passage: 1Kor 3:16-18, Efe 5:25-26

Kanisa ni nini? Zipo tafsiri nyingi juu ya hili jambo na kwa ufinyu wa maelezo ya kweli wengi huamini kwamba kanisa ni jengo au nyumba ya ibada, lakini maandiko matakatifu yenyewe yanatueleza kanisa au ilo jengo (hekalu) la Mungu ni sisi yaani miili na mioyo yetu na Mungu anaishi ndani yetu 1Kor 3:16-18. Kwa kuwepo kwa upotofu wa kimaana juu ya kanisa imepelekea kuwa na ongezeko kubwa la majengo ya ibada na kwa majina mbali mbali na yote yanatambuliwa kama makanisa. Kwa kulifahamu hilo ndugu jeff anatuweka wazi na kutupa utambuzi juu ya hilo, pia naye anakubali na kukiri kwamba miongoni mwa hayo makanisa huwezi kulikuta kanisa ambalo limekamilika kwani yote hayo yanahusisha wanadamu, iwe kiuongozi hata mafundisho yenyewe.

Katika somo hili ndugu Jeff anatupa aina nne (4) za makanisa mbali mbali ili tuweze kua na maamuzi katika kuifuata kweli. Kuna makanisa ambayo yana mambo ya kidunia, yapo ambayo ya kushika sheria, yapo ambayo yana ibada za misisimko pia yapo ambayo yanaabudu sanamu. lakini katika yote hayo ndugu jeff anatukumbusha jukumu letu sisi kama waamini wa kweli ya Kiristo na kanisa lake la kweli apa duniani ni nini tunapaswa kufanya kutokana na maagizo kutoka kwenye Biblia. Efe 5:25-26 “Enyi waume, wapendeni wake zenu, kama Kristo naye alivyolipenda kanisa, akajitoa kwa ajili yake; Ili makusudi alitakase na kulisafisha kwa maji katika neno;

Mafundisho haya yanaendana na masomo yanayopatikana katika Kozi ya Maji ya Uzima inayoitwa Nyayo za Kristo. Kwa maelezo zaidi kuhusiana na masomo haya au kujiunga na kozi wasiliana nasi kupitia

Barua pepe: neno@majiyauzima.com

Simu: +255754 490 549 / +255694 298 395 / +255719 275 767

Tovuti: majiyauzima.com