17 Kristo na Kujitenga na Dunia; Uko Kwenye Ufalme Upi? (Nyayo za Kristo)

17 Julai, 2025

Kitabu: 2 Korintho

Bible Passage: 2 Kor 6:17-18

Dunia ni nini? Zipo maana nyingi juu ya dunia, zipo za kisayansi pia za kihistoria. Lakini katika imani tunaamini kwamba dunia ni mbaadala wa mbingu yaani kuna duniani na kuna mbinguni, maana hii inapata uzito kiimani kwani tunaamini mwanzo wa yote Mungu alikua mbinguni na bado yupo mbinguni na akaamua kuiumba dunia na kuwaweka wanadamu ndani yake, na wanadamu wakamuasi na kuwa na mambo yao ya kidunia ambayo yanapingana na mapenzi ya Mungu.

Kwa kuielewa maana hii vizuri ndugu Tim anatufundisha kwamba kwa sababu hayo mambo ya kidunia yanapingana na Mungu na sisi ambao ni wafuasi wa Kristo na tunamtumainia Mungu, hivyo hatuna budi kujitenga nayo, na alitueleza mambo hayo ni kama zinaa, rushwa, mauaji, ufisadi, tamaa, chuki, husda na mengi mabaya yafananayo na hayo na hakuishia hapo pia alitueleza ni yapi yatupasa kufanya ili kumtukuza Mungu ni kuwapenda ndugu na maadui pia, kufanya ibada, kujitoa katika huduma na mengi mema yafananayo na hayo.

Binafsi naye alikiri ya kwamba si rahisi kujitenga na shughuli hizo za kidunia, kwani sisi ni wanadamu. lakini akatusihi kwamba tukijitenga na ya hapa duniani yapo mengi mazuri ambayo tutayakuta mbinguni kwa Mungu.na akatutia nguvu kwa nukuu ya kibiblia juu ya hili 2 Kor 6:17-18 “Kwa hiyo, Tokeni kati yao, Mkatengwe nao, asema Bwana, Msiguse kitu kilicho kichafu, Nami nitawakaribisha. Nitakuwa baba kwenu , Nanyi mtakuwa kwangu wanangu wa kiume na wa kike, asema Bwana Mwenyezi”.

Mafundisho haya yanaendana na masomo yanayopatikana katika Kozi ya Maji ya Uzima inayoitwa Nyayo za Kristo. Kwa maelezo zaidi kuhusiana na masomo haya au kujiunga na kozi wasiliana nasi kupitia

Barua pepe: neno@majiyauzima.com

Simu: +255754 490 549 / +255694 298 395 / +255719 275 767

Tovuti: majiyauzima.com